Thursday, August 9, 2007

REPUBLIC OF TAMBAZA

MUHTASARI WA KIKAO CHA KWANZA CHA WALIOSOMA TAMBAZA

Tarehe: Agosti 4, 2007
Mahali: Rose Garden, Dar-es-Salaam – TANZANIA
Muda: Saa 11:00 jioni mpaka saa 12:30 jioni
Mahudhurio
1. Herieth Koka 1999-2001 Mwenyekiti

2. Alex Mayunga 2000-2002 Katibu

3. Kassongo Abedi 1992-1995 Mjumbe

4. Khalid Bitebo 1992-1995 Mjumbe

5. Elia Yobu 1998-2000 Mjumbe

6. Vivian Samweli 1999-2001 Mjumbe

7. Eric Ongara 1999-2001 Mjumbe

8. Liginiku Milinga 2000-2002 Mjumbe

9. Elly Mgumba 2000-2002 Mjumbe

10. Rehema 2000-2002 Mjumbe

11. Yuster 2000-2002 Mjumbe

12. Rehema 2000-2002 Mjumbe

Wajumbe wa kikao waliazimia kuanza kikao saa kumi na moja kamili baada ya kuona muda unazidi kusonga. Kabla ya kuanza rasmi kwa kikao, wana jumuiya walijitambulisha majina, miaka na shughuli wanazofanya kwa sasa
Herieth Koka alipendekezwa kuwa Mwenyekiti wa kikao na Alex Mayunga kuwa Katibu wa kikao.
Baada ya kupitisha Mwenyekiti na Katibu vipengele vya ajenda za kikao vilisomwa na Mwenyekiti na kupitishwa kama sehemu za ajenda ya kikao.

VIPENGELE VYA AJENDA
1. Uanzishwaji wa jumuiya ya Wana Tambaza
2. Kubuni Mchakato wa jina la Jumuiya
3. Kubuni mchakato wa usajili wa jumuiya na muongozo.
4. Ushiriki wa Wanajumuiya walio nje ya Dar-es-Salaam na nje ya Tanzania
5. Jinsi ya kuongeza wanajumuiya
6. Mengineyo

UANZISHWAJI WA JUMUIYA YA TAMBAZA.
Katibu alianza kueleza chimbuko la uanzishwaji wa wanajumuiya ya Tambaza. Kwanza alitambua harakati mbalimbali ambazo zilikwishafanywa mara kadhaa na baadhi ya Wahitimu waliomaliza Tambaza miaka ya nyuma.
Vuguvugu lilipata kasi kipindi cha majuma manne yaliyopita kupitia katika mijadala ya barua pepe miongoni mwetu.
Moja wapo ya barua pepe ilikuwa ikifanya rejea kwa maneno ya Mwalimu Nyerere yanayopatikana katika ofisi za Shule ya Tambaza. Katika ujumbe ule wa Mwalimu Nyerere ulimfananisha mtu anayepata elimu kama mtu aliyetumwa na kijiji chenye njaa kupewa kidogo kilichopo kwa matumaini ya wanakijiji kupata mavuno.
Tafakuri hii ilitumwa kwa baadhi ya watu kujihoji kama baada ya wao kupewa mbegu na wanakijiji wale ana chochote alichoweza kukirudisha. Mwelekeo wa mijadala ulionesha kwamba “kijiji” tajwa ni shule tuliyopita yaani Tambaza. Je kuna anayekumbuka nyuma tuliacha nini?
Hii ikachochea wanajumuiya kuzidi kualika kwa kutegemea barua pepe ambazo mtu alikuwa nazo za wana-Tambaza.
Barua pepe ilikuwa nyenzo kuu ya kupashana ujumbe. Wanajumuiya wenye Blogu kama Maggid Mjengwa, Elly Mgumba na Said Yakub walitumia blogu zao kama jukwa la wanajumuiya kupashana habari na mara nyingi kutiana hamasa.
Mjadala huu ndio uliozaa kikao hiki cha kwanza baada ya wajumbe wengi kupendekeza hivyo

KUBUNI MCHAKATO WA JINA LA JUMUIYA
Kikao kilitaarifiwa kwamba Alex alibuni jina la Republic of Tambaza kama njia ya kutoa hamasa kwa wana jumuiya kuwasiliana. Jina hili halikuwa rasmi na vivile ilionekana na baadhi ya wajumbe kwamba halivutii sana na linaweza kujenga taswira hasi situ ambacho wanajumuiya wote hatuko tayari.
Kikao kilipendekeza Mwezi wote wa Agosti utumike kubuni jina la wana jumuiya. Mwisho wa kutuma majina kwenye orodha ya barua pepe ni Agosti 30 mwaka huu.
Katika kikao hicho majina yafuatayo yalipendekezwa.

Elly-TAMBAZAMANI

Liginiku -Tambaza Society

Herieth-Tambaza Alumni

Vivian-Tambaza Viva

Alex- We-Tambaza

Yuster-Tambaza Community

Elly-Ex – Tambaza

Alex-Tambaza Foundation


KUBUNI MCHAKATO WA USAJILI WA JUMUIYA NA MUONGOZO
Wajumbe wa kikao walipendekeza jumuiya isiwe kama mkusanyiko wa vatu tu badala yake ipate usajili. Hii ilitokana na dhamira ya kuja kusaidia “kijiji chetu” cha Tambaza. Ili kupata uhalali wa kisheria na kiutendaji ilipendekezwa jumuiya kwa jina litalopendekezwa isajiliwe kama Kampuni isiyozalisha faida chini ya msajili wa Kampuni (BRELA).
Alex na Liginiku walipewa jukumu la kufuatilia taratibu na gharama za usajili wa kampuni zisizozalisha faida na wawe wamemaliza jukumu hilo ifikapo tarehe 10 Agosti 2007.

4. USHIRIKI WA WANAJUMUIYA WALIO NJE YA DAR-ES-SALAAM NA NJE YA TANZANIA
Wajumbe walizingatia umuhimu wa kuwa na jumuiya huru kwa kila aliyepata kusoma Tambaza hata akiwa pembe yoyote ya Dunia. Kwa kuanzia njia za mitandao ya simu na intaneti ndio njia rahisi zaidi za kuwashirikisha katika kila hatua za michakato hii. Wajumbe walitaarifiwa lengo la Ndugu Chacha kufungua tovuti kwa ajili ya wanajumuiya.
Wajumbe wamependekeza Mwanatambaza Chacha aanze jukumu hili baada ya nawasilisho ya muhtasari huu kusambazwa kwa wanajumuiya.
Maoni ya nini na jinsi gani kiwepo yanakaribishwa kwa kila mwana jumuiya ili kuwa na tovuti inayovutia na iliyo hai.
Bwana Chacha ameombwa kuratibu orodha ya barua pepe (e-mail list) na kubuni njia ya kuifanya active, ikiwezekana atengeneze email group kwa kuanzia..
Ilitolewa rai wajumbe wa-scan picha zao wakati ule wakiwa shule na kuzituma kwa Chacha, Maggid, Yakub na Elly kwa ajili ya kukumbushana wanajumuiya. Hii itavuta kumbukumbu zaidi na kuweza wanajumuiya wengine wako papi wanajishughulisha na nini.
Siku za usoni tutabuni njia bora zaidi ya kuweka mahusiano katika ya jumuiya na walimu na wanafunzi wa Shule ya Tambaza. Kwa njia hii tutaangalia mgawano wa majukumu kati ya wanajumuiya walio nje ya nchi na ndani ya nchi (Dar-es-Salaam na nje ya Dar-es-Salaam.
Jumuiya itafungua Joint Account Ambayo wajumbe watashauri mchakato bora zaidi wa kuendesha akaunti ya pamoja kwa kuwa chombo hiki ni cha wote waliopata kusoma Tambaza.

JINSI YA KUONGEZA WANAJUMUIYA
Wajumbe wa kikao walitoa rai kwa kila mwanajumuiya kuweza kusambaza ujumbe kwa marafiki na jamaa wote waliopata kusoma Tambaza. Siku za usoni tutatoa matangazo katika vyombo vya habari.

MENGINEYO
I. Ilikubaliwa kwamba uongozi wa shule ushirikishwe katika hatua za mwanzo za mchakato huu. Ilipendekezwa wajumbe wafuatao wawasiliane na uongozi wa shule ili kuwataarifu azma na dhamira ya wanajumuiya.
Wana Tambaza watawakilishwa na ujumbe wa:
i. Herieth
ii. Alex
iii. Kassongo
iv. Elia
v. Yuster
Wajumbe wanakusudia kuomba shule isaidie kupata majina ya viongozi mbalimbali wa kisiasa na watu toka kada mbalimbali ili tuweze kuwaalika katika jumuiya.

II. Uongozi wa Muda
Wajumbe walitwateuwa Mwenyekiti na Katibu wa kikao kuwa viongozi wa muda na sehemu iliyobaki kuwa wajumbe wa kamati ya muda ya jumuiya.

III. Herieth alijitolea kuwasiliana na uongozi wa shule ifikapo Alhamisi ili kuomba ahadi ya kukutana na ujumbe.
IV. Wajumbe wanawashukuru Maggid Mjengwa, Elly Mgumba na Said Yakub kwa kutoa fursa kwa blogu zao kutumika kahamasisha wanajumuiya. Aidha tunaomba waendelee na moyo huo wa kizalendo ikiwa ni pamoja na kubandika muhtasari huu wa kikao na shughuli nyingine zijazo.
V. Wajumbe walipendekeza kikao kingine kifanyike tarehe 2 Septemba 2007. Imependekezwa kikao hiki na vingine vyote vijavyo vifanyike shule ya Tambaza.
VI. Wajumbe watume maoni kwa Chacha juu ya muundo wa tovuti.

No comments: