Monday, August 6, 2007

21 DAYS OF YELLO CARE


21 Days of Yello Care ni programu ambayo imebuniwa na kampuni ya MTN ili kuhakikisha kua wanarudisha fadhila kwa jamii ambayo wanaitumikia, katika kipindi hiki cha majuma takribani 3 wafanyakazi wa MTN bila kujali vyeo wala nyadhifa hushiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu. Kuna mambo kama matano au sita yanayofanywa kwenye programu hii, kupaka rangi blackboards na kusaidia shule zisizojiweza kwa kuwapa misaada itakayosaidia kwa njia moja au nyingine, kutembelea wagonjwa na watoto yatima, kuwasaidia na kuwafariji, kuchangia damu n.k, hakika ni zoezi la kuigwa na makampuni ya hapo nyumbani kama bado hawafanyi hivi.

No comments: