Monday, July 23, 2007

BADO TUNA MATUMAINI

Haya tena, kwa wale wasionijua ngoja niweke mambo hadharani, mimi ni mnazi mkubwa wa Mashetani Wekundu, Saga la Teves bado linaendelea huku mimi pamoja na wanazi wote wa MAN UTD tukiwa na mategemeo lukuki ya kumnyakua nyota huyo wa Kiajentina.
Mpaka sasa shirikisho la kabumbu duniani FIFA pamoja na wawakilishi kadhaa wa shirikisho la soka Uingereza ndio wenye dhamana ya kutegua kitendawili hicho. Ki ufupi ni kwamba tukimpata huyo basi msimu ujao tutatisha, hakuna cha bwawa la maini wala filigisi. Ni hayo tu.
Source; BBC News

No comments: